Close

Not a member yet? Register now and get started.

lock and key

Sign in to your account.

Account Login

Forgot your password?

Interview with Mo Dewji's blog - Nov 2009

 

Tuanze kwa kukushukuru kwa kukubali kuzungumza na blog yetu. Karibu sana!

Nashukuru kwa fursa hii. Hii ni mara yangu ya kwanza kabisa kufanya interview. Lakini nimekubali kufanya hii kwa sababu tatu:

1. Mo ni rafiki yangu na nimefurahi kwamba ameamua kuanzisha blog. Aliponieleza nia yake hii miezi kadhaa iliyopita, niliahidi kumsapoti kwa njia yoyote ile . Sasa kwa kuwa amesisitiza sana kwamba njia ya kumsapoti ni kwa mimi kufanya hii interview, baada ya mimi kusita sana, nikaona nitimize ahadi yangu, lakini nikiwa bado naamini kwamba sijafika mahali pa mimi kustahili interview kuhusu maisha yangu. 

2. Nimefurahi amekubali ombi langu la kutozungumzia masuala ya kisera au mambo yanayohusiana na undani wa kazi ninayoifanya sasa. Hii imefanya mambo yawe rahisi.

3. Nilidhani ni muhimu wengi wetu, hasa vijana, tukaonyesha imani na njia hii mpya ya kupashana habari (blog), hata kama ni kwa kufanya mambo ambayo hatukuwahi kuyafanya huko nyuma kudhihirisha kwamba tunaiheshimu na kuipa umuhimu medium hii mpya. 

Tungeanza na wewe kutupa historia yako (Elimu, Kazi, Maisha kwa ujumla):

Nilizaliwa tarehe 28 Januari 1974. Nalipenda sana jina langu kwasababu mara nyingi ninapojitambulisha kwa watu, automatically linaanzisha mazungumzo. Mara nyingi huulizwa kama nilizaliwa mwezi Januari ndio maana nikapewa jina hilo. Ukweli ni kwamba hiyo sio sababu per se. Sababu kubwa ni kwamba, wakati nazaliwa, Mzee wangu alikuwa na rafiki yake mkubwa aliyempenda sana aliyeitwa Januari. Akaamua kunipa jina lake kwa mapenzi yake kwa rafiki yake. Ilikuwa ni coincedence tu kwamba nilizaliwa mwezi wa kwanza. Lakini jina ambalo Babu yangu mzaa baba alinipa na alipenda kuniita kabla hajafariki mwaka 1984 ni Rajab, ambalo ni jina lake yeye. Kwahiyo hadi leo, kijijini kwetu Mahezangulu, Lushoto, hasa kwa wale wazee wa kule, na hata kwa bibi yangu, najulikana kama Rajab.

Nimesoma kwenye shule mbalimbali za msingi katika mikoa mbalimbali nchini, kadri wazazi wangu walivyohama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine. Nilianzia Monduli mwaka 1981. Mwaka 1983, nikapelekewa kukaa na bibi mzaa mama kijijini Kituntu, karibu na Kyaka, Bukoba Vijijini. Mama yangu kwao amezaliwa peke yake, kwahiyo bibi alihitaji mjukuu wa kukaa naye kumsaidia. Ndio nikatolewa kafara. Hahahaha! Kwahiyo darasa la tatu, la nne na la tano, nimesoma kijijini. Siwezi kusahau maisha yale: asubuhi ni kupiga umande literally kwenda shule umbali wa kama kilomita nne na nusu hivi kutoka nyumbani, ukirudi saa tisa ni kwenda kuchunga mbuzi, ukisharudisha mbuzi zizini saa kumi na mbili jioni ni kwenda kuchota maji mtoni, usiku kazi ni kumsaidia bibi kuuza pombe ya ndizi inayoitwa lubisi (bibi alikuwa na kilabu maarufu pale kijijini).

Samahani hapa nime-digress kidogo kwa kukumbuka na kuelezea zaidi kipindi hiki. Lakini experience hii ni sehemu ya mimi. Siku hizi NGOs zinayaita haya “mazingira hatarishi”, lakini watoto wengi vijijini ndio maisha yao ya kila siku. Some make it, through pure luck or strength of character, some don’t. 

Anyway, nilirudi kukaa na wazazi wangu tena wakiwa Lushoto kwahiyo nikasoma darasa la sita pale, Shule ya Msingi Kitopeni, na kwenda kumalizia darasa la saba shule ya Msingi Masiwani Tanga Mjini. Hapa Tanga Mjini niliingia na kusoma madras which was quite rewarding ingawa sikumaliza msahafu. Pamoja na kuhamahama, na dhahama za maisha ya kijijini, I have always done well in school. Sikumbuki kama nilishawahi kushuka chini ya nafasi ya nne.

Form one nilisoma Handeni Secondary School, hii ilikuwa ni shule mpya, sisi tulikuwa Form One wa pili – kulikuwa hakuna walimu, madawati, maabara, n.k. Form Two hadi Form Four nikasoma Galanos, Tanga Mjini. Wakati nikiwa Form Three nilichaguliwa Deputy Head Prefect pale Galanos. Form Five na Six nikawa Forest Hill Secondary School, Morogoro, ambapo siku ya graduation nilitunikiwa cheti cha Overall Best Student.

Anyway, wakati nasuburi kwenda university, nikaenda kutafuta kazi kwenye kambi za wakimbizi Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma. Nikafanikiwa Kasulu. Ukiacha maisha ya kijijini na bibi, this was another rewarding experience kwenye maisha yangu. Nilipata responsibilities kubwa kadri muda ulivyoenda, hadi kufikia ngazi ya Assistant Camp Manager kwenye kambi ya Mtabila Extension au Mtabila II, ambayo literally niliianzisha mimi (baada ya kuwa Serikali imetoa eneo) from the scratch kwa maana ya kusimamia infrastructure na kugawa plots kwa wakimbizi. Kwenye kazi hii ndipo kwa mara ya kwanza nilipokutana na kuanza ku-engage na kujenga urafiki na watu wa mataifa mbalimbali waliokuwa expatriates kwenye camps. Muda wa kwenda Chuo ulivyofika, sikwenda kwani nilinogewa na kazi, mwaka uliofuatia sikwenda tena kwani nilipata responsibilities kubwa zaidi kambini and I was making and saving good money.

Eventually nikapata Chuo Marekani. Nilianza Boston baadaye nikajiunga na St. John’s University Minnesota. Hiki ni Chuo cha Wakatoliki Wabenedicto kilichokuwa katikati ya pori na lakes, a very beautiful and quiet place, katikati ya Jimbo la Minnesota. Pale, degree niliyochukua ni BSc in Peace and Conflict Studies. Niliamua kusoma hii kozi kutokana na experience yangu kwenya makambi ya wakimbizi. Nilitaka kuelewa ni kwa namna gani tunaweza kuzuia watu wasikimbie kabisa nchi zao, kwani maisha ya ukimbizi, kwa nilivyoyaona, ni ya udhalilishaji mkubwa sana na yanaondoa dignity ya mtu.

Wakati nikiwa St. John’s University, nilirudi tena kufanya research yangu na UNHCR kwenye makambi ya wakimbizi Kasulu na Kibondo lakini pia kwenye way stations ndani ya Burundi na DRC.

Baada ya kumaliza St. John’s, nikapata research assistantship kwenye ofisi ya Rais wa zamani wa Marekani, Mzee Jimmy Carter, Carter Presidential Centre, kule Atlanta, Georgia. Kazi hiyo ilinipeleka hadi kufanya kazi Sierra Leone, ambako pia nilijifunza mengi. Pia Atlanta ndiko nilikofanikiwa kukutana na mke wangu mpendwa, Mona, ambaye mwakani itakuwa miaka kumi tangu tujuane, na ambaye, pamoja naye, tuna mtoto mmoja wa kike wa miaka mitatu na nusu anayeitwa Jasmin.

Baada ya pale nikajiunga na George Mason University, iliyoko maeneo ya Fairax, Washington DC metro area, kusoma Masters kwenye fani ile ile ya diplomasia na usuluhishi wa migogoro. Nilikuwa a very active graduate student kwa maana ya kushiriki mijadala na professional and advocacy associations mbalimbali pale DC. I created a vast network of friendships pale ambayo hadi leo nafaidika nayo. Nikiwa graduate school, nilipata fursa ya kufanya internship Wizara ya Mambo ya Nje.

Baada ya kumaliza graduate school nikawa-recruited Serikalini na kuajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama Afisa wa Mambo ya Nje Daraja la Pili. Nikiwa pale, nilipata fursa ya kufanya kazi kwa karibu na Waziri wetu wakati ule, hasa kwenye harakati za kutafuta suluhu ya mambo ya Burundi na DRC. Kwahiyo, wakati alipoamua kugombea Urais, akaniomba nichukue likizo isiyo na malipo Serikalini nisaidie kuwa errand boy kwenye kampeni yake, ku-organise makaratasi na notes zake, na kuchangia hapa na pale kwenye tafakuri za kuendesha na ku-organise kampeni yake wakati ule. Tulifanikiwa kufanya mambo mengi mapya na ya kisasa kwenye kampeni ile. Nilishukuru sana kupata fursa ya kuzunguka kwa njia ya barabara katika kila kona ya nchi hii, Mikoa yote na Wilaya zote na kujua kwa kina changamoto na fursa za maendeleo katika maeneo yote. Alipofanikiwa kuchaguliwa, akaniteua nije kumsaidia hapa Ikulu na hapa ndipo nilipo hadi leo.

Kazi hii ni ya heshima kubwa sana na ni muhimu kui-approach with humility. In fact, kuna nyakati natafakari sana kwamba, katika kufanya kazi hii, inawezekana nafaidika zaidi mimi katika kujifunza kuhusu nchi yetu, Serikali inayoendeshwa, maamuzi yanavyofanywa, sera zinavyotengenezwa, na siasa na uongozi wa nchi kwa ujumla unavyoendeshwa, kulivyo Rais anavyofaidika na usaidizi wangu. 

Wewe ni mtoto wa mwanasiasa,(Mh. Yusuph Makamba), je unafikiria kuna mategemeo makubwa yanayokuja kama dhamana ukizaliwa kwenye familia maarufu ya kisiasa kama ya Makamba?

Kwanza kuna heshima kubwa kutambua kwamba mzazi wako ameyatoa maisha yake kwa utumishi wa umma. Kuna sacrifices ambazo kama familia lazima mzikubali kutokana na shughuli za Mzee.

Pili, kuwa na jina la Makamba kuna uzuri na ubaya wake. Uzuri wake ni kwamba wapo watu wengi katika sehemu mbalimbali za nchi hii ambao wamefanya kazi na baba na wanamheshimu sana. Kwahiyo tayari unayo network kubwa ya extended family ambao wengi wanakujua tangu uko mdogo na wanafurahishwa na wanajiona ni sehemu ya mafanikio yako, na wako tayari kukusaidia kwa ushauri au mambo mengineyo wakati wowote.

Lakini pia wapo ambao wanaona Mzee Makamba ni mtu fulani hivi hafai au mtu wa hovyo au wana kutokuelewana naye kimitizamo au kisiasa. Mara nyingi, katika mazingira ya kwetu hapa, hawa watu hawawezi kutofautisha kati ya baba na mtoto. Kwahiyo, unajikuta unarithi marafiki na maadui wa baba yako hata bila ya wewe mwenyewe kutaka.

Vilevile, ukiwa mtoto wa mwanasiasa mara nyingi kuna dhana katika jamii yetu kwamba umeishi a privileged life na kwamba umeharibika au umedekezwa na kwamba huwezi kujisimamia mwenyewe. Hii si kweli. Maisha yetu sisi miaka yote yamekuwa ya kawaida sana. Nakumbuka Mzee wangu kwa mara ya kwanza amemiliki nyumba yake si muda mrefu uliopita, na ilikuwa ni nyumba ya makuti pale kijijini Kiomoni, Tanga. Wakati wa mvua, nyumba hii ilikuwa inavuja. Tunahamisha vitanda na furniture. Na wakati tunakaa Kiomoni tulikuwa tunasoma Masiwani, Tanga Mjini ambapo ni Kilomita 12, na tulikuwa tunaenda kwa mguu, ukibahatisha ni baiskeli, na lunch ilikuwa ni mihogo ya kuchoma na maji, mama alikuwa anatupa shilingi hamsini kila asubuhi. Lakini leo kila mtu anadhani maisha yako yote umekula mkate na siagi na umepelekwa shule kwa gari. 

Jambo jingine, ni kwamba kwa kutoka kwenye familia ya mwanasiasa, kwenye jamii yetu kuna perception kwamba mafanikio yako yote ni lazima umeyapata kwa kubebwa. Hata kama uwe na uwezo kiasi gani, hata kama uwe unachapa kazi kwa kiasi gani, utasikia “aaah, watoto wa wakubwa wale”. Basically, juhudi zako hazionekani. Lakini hili halisumbui sana kwa sababu kwa bahati nzuri wale wanaosema haya ni wale ambao hawajawahi kukutana na wewe au kufanya kazi na wewe. Wanaokujua as a person or a colleague wanatambua ukweli.

Pia kuna hii habari naulizwa kila siku kwamba unajisikiaje kumsoma Mzee wako kwenye magazeti kila siku kwa wale wanaomsifu na kwa wale wanaomponda. Ukishakuwa kwenye familia ya siasa, haya mambo unayazoea, na hayakusumbui wala kukunyima usingizi. Unasoma headline, ukifungua ukurasa wa pili wa gazeti ndio habari imeshakwisha, maisha yanaendelea kama kawaida.

Mwisho wa yote, dhamana kubwa ni kujitambua na kujiamini na kujua unachofanya, lakini pia na kutambua kwamba kila utakachofanya, hasa mambo ya hovyo, implications zake sio kwako tu, bali pia kuna implications za kisiasa kwa mzazi wako.

Kuna tetesi kuwa unataka kujiingiza kwenye siasa na hasa inasemekana unataka kugombea ubunge mwaka ujao, Je habari hizi ni za ukweli?

Tetesi hizi zimekuwepo tangu mwaka 2005. Ikifika wakati muafaka nitalizungumzia jambo hili.

Hata hivyo, nimekuwa nawashawishi, na nawasaidia kwa kadri ninavyoweza, vijana wengi kuingia kwenye utumishi wa umma, sio tu kwenye siasa, bali hata Serikali kwa ujumla kwa kuwa naamini kuna a sense of responsibility kwa generation yetu na sisi ku-step up.

Tuelezee nchi ambazo umezitembelea duniani na ni mambo gani umejifunza huko unayoweza ku-share na vijana.

Kila sehemu tunayokwenda najaribu kupata muda kujifunza historia ya pale, siasa za nchi ile, changamoto za maendeleo walizonazo, na mambo wanayofanya kukabiliana nazo. Sidhani kama nafasi hapa inaruhusu kuelezea yote haya kwa nchi zote nilizopata kutembelea. Labda nielezee tu sehemu mbili ambazo tumetembelea hivi karibuni na mambo ambayo nimeyaona kama mimi binafsi – ambayo hayahusiani na shughuli za Kiserikali.

Wiki kadhaa zilizopita nimekuwa Cairo na Roma. Miji hii miwili ina historia kubwa kwa civilisation na dini zetu kuu mbili Uislam na Ukristo. Nilipopata muda mchache wa mapumziko, nijaribu kuzunguka kwenye landmarks na museums. Ukipitia landmarks za Roma – the colosseum, the panthenon, kanisa la Mt. Peter, mabaki ya ukuta wa old Roma, na sehemu nyingine nyingi - unajifunza kuhusu statecraft, historia ya Ukristo, ujenzi wa Himaya ya Roma, na mambo mengineyo mengi. Ukiwa Cairo, kwa kwenda kwenye pyramids, kutembelea the Citadel, misikiti ya zamani ya Sultan Hassan na Sultan Ali, na kwenda kwenye national museum yao kupata maelezo ya kuhusu maisha ya Pharaohs, unajifunza kuhusu historia ya dini zote, unashuhudia landmarks zinazotajwa kwenye Biblia na Kuran, unajifunza kuhusu Himaya ya Ottoman, na nyinginezo zilizopata kutawala Egypt, basically Egyptology yote unaiweka kiganjani. Kwahiyo unajifunza mengi, ikiwa pamoja na umuhimu wa taifa ku-preserve historia yake na ya watu wake kama msingi wa kujenga pride na uzalendo wa watu kwa nchi yao – lakini vilevile kujenga a soul of a nation.

Hata hivyo, najivunia zaidi na fursa niliyopata ya kuzunguka nchi yetu yote – kila kona kwa barabara – mara mbili: wakati wa kampeni na wakati nikifanya kazi hii niyayoifanya sasa. Nimejifunza mengi kuhusu nchi yetu, watu wake, na changamoto zake na fursa zilizopo za mabadiliko katika maisha yao. I will always be grateful kwa Mhe. Rais kwa fursa hii. 

Wewe unajuana na unabadilishana mawazo na watu wengi nchini, ni viongozi gani nchini unafikiri ni mfano kwa vijana wanaofikiria kufuata nyayo zao kwenye siasa?

Wapo viongozi wengi walioitumikia na wanaoendelea kuitumikia nchi hii kwa uadilifu, kwa bidii, na kwa heshima mkubwa. Vijana hawawezi kupata shida katika kuchagua kati ya hao ni wapi wafuate nyayo zao.

Ni muhimu pia kutambua ni kwamba vijana wengi wanahamasika kuingia kwenye siasa kutokana na mafanikio ya vijana wa rika lao waliowatangulia kwenye siasa. Kwahiyo, ni muhimu sana kuwaunga mkono na kuhakikisha kwamba vijana wenzetu walioingia kwenye siasa, katika vyama vyote vya siasa, wanafanikiwa na wanafanya vizuri ili wengine nao wahamasike na waone kuwa inawezekana.

Hata hivyo, nadhani fursa za kuitumikia nchi na kushiriki kwenye mabadiliko sio lazima ziwe ndani ya siasa peke yake. Wako vijana wengi mjini hapa wanafanya mambo makubwa sana kwenye nyanja finance, kwenye kwenye ICT, kwenye NGOs ambao tayari ni leaders kwenye maeneo hayo. Kuna firm hapa mjini inaitwa Serengeti Advisers ya rafiki zangu kina Aidan, Bertram, Abdu pamoja na vijana wengine pale kina Chiume, Bakilana, Eneza – they are doing great things. Yupo pia rafiki yangu Rashid Shamte na vijana wenzake pale Push Mobile/Sixtelecoms. Na hawa nao pia tujaribu kufuata nyayo zao na tuwa-recognise pia kama viongozi, sio tu wale waliopo kwenye politics au wanaotaka kuingia kwenye politics.

Wewe ni kati ya vijana wanaobahatika kwenda nchi mbalimbali na kuwaona viongozi mbalimbali, ni kiongozi gani wa kimataifa unayemkubali kwa kazi yake?

Kila kiongozi anakabiliwa na changamoto mahsusi kulingana na hali, mazingira na nyakati ambazo nchi yake inapitia. Kwahiyo ni vigumu kuwapima viongozi wote duniani kwa rula moja. Vilevile, ni vigumu kuwapima viongozi ambao hawajamaliza muda wao madarakani kwasababu kwenye uongozi wa juu wa nchi, historia inaandikwa kila siku.

Je unaye role model ambaye amekuhamasisha au anakuhamasisha kupiga hatua mbele na kufika mbali kimaendeleo?

Ninao wawili. Wa kwanza ni baba yangu, Mzee Makamba. Ningependa nami niwe mzazi mwema kama alivyo yeye. Anaipenda familia yake, anajali sana ndugu hata wawe ni wa mbali kiasi gani, hakosi msiba wala harusi, hadanganyi hata kidogo, anaridhika na maisha yake ya kawaida, anajiamini, haogopi wala hatishwi na mtu, hakosi usingizi kwa criticism au kusemwa, anasema kile kilicho moyoni mwake, na haweki kinyongo na maisha yake ni ya furaha wakati wote. Kwasababu yuko hivyo, na sisi wanae tunahamasika kuwa hivyo. Na yuko tayari kujinyima na kujibana ili tusome na tujiendeleze. Na nadhani ana ka-store ka stories kama 3,000 hivi, na wakati wowote yuko tayari kuchomoa story yoyote ya kuvunja mbavu au ya kufundisha ambayo ni relevant kwa mazungumzo yanayoendelea.

Wa pili ni Rais Kikwete. Sijapata kukutana na mtu mwenye passion kuhusu maendeleo ya nchi na watu wake kama alivyo Rais. Ana bidii kubwa sana ya kazi wakati mwingine anaji-push kupita kiasi. Kama binadamu, ni mtu mwema sana. Na anapenda mambo yafanyike kwa viwango vya juu. Katika mazingira tuliyonayo sasa, tumepata bahati kuwa na kiongozi wa namna hii, ambaye uhuru wa watu kusema haumsumbui, na ambaye yuko confident in his own skin. Amefikia kile ambacho Dag Hammarskjold anaita “a maturity of mind”, ambapo watu wachache sana katika uongozi wanaweza kukifikia – fearlessness and capacity to endure uncertainty.

Muda wako wa mapumziko unautumiaje?

Muda wa mapumziko kwa kazi hii ni mara chache kuupata. Lakini ninapopata mara nyingi hukaa na familia kidogo. Mke wangu na mimi hupenda sana sinema, tangu tumejuana tulikuwa tunaenda sinema kwahiyo tunafanya hivyo hapa pia pale Mlimani City, tatizo ni kwamba wanachukua muda sana kuweka new releases.

Lakini pia nina interests kadhaa, hasa muziki na kusoma vitabu. Ni mwanachama wa a very vibrant reading group hapa Dar ambapo tunakutana kila mwanzo wa mwezi kujadili kitabu au article ambayo imechaguliwa kwa mwezi huo. Pia ni mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Tanzania House of Talent. Nashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii. Kwahiyo, nikipata mapumziko najikuta niko busy tena na mambo mengine ya kukutana na watu.

Lakini pia napenda kukaa na marafiki na kupiga story. Mo anajua, nikiwa around tunakutana kwa kahawa na kujadili mambo ya siasa, uchumi, maendeleo na ustawi wa vijana wa nchi yetu.

Tumesikia na tumeona kwenye blog yako kwamba wewe ni mtu wa kupenda vitabu. Ni vitabu vya aina gani? Na je sasa hivi unasoma kitabu gani. Na vitabu gani, masuala gani ya jumla, unaweza ku-recommend kwa vijana kutafakari na kujifunza?

Ni kweli, nina passion na vitabu na hakuna wakati ambapo sisomi kitabu. Kwa jumla niko interested na topics zote. Ukija kwenye kamaktaba kangu nyumbani utakutana collection ya a range of topics kuanzia Matt Ridley’s biography ya Francis Crick, hadi Mariama Ba’s So Long a Letter, hadi Emmanuel Levinas’ Totality and Infinity, hadi Frans de Waal’s Chimpanzee Politics. So, I am very indiscriminating in what I choose to read.

Hata hivyo, kwenye kuchagua vya kusoma ninakuwa driven na interest za wakati huo. Kuna kipindi, kwa miezi hadi sita, nakuwa so fixated na topic fulani, labda public health, basi nakuwa nasoma vitabu au literature thoroughly kuhusu public health. Baadaye, kwa kuhamasishwa na some article or a conference or a great conversation or a documentary, naanza something else.

Kwa sasa, niko obssessed na hii idea ya economic development na kwanini nchi zinatofautiana kwa hatua na kasi ya maendeleo. Kwahiyo, nasoma vitabu viwili kwa mpigo sasa (mimi ni mmoja wa wale wenye tabia mbaya ya kusoma vitabu viwili kwa mpigo): How Rich Countries Got Rich and Why Poor Countries Stay Poor, kimeandikwa na Erik Reinert na kingine ni Kicking Away the Ladder: Development Strategy in Historical Perspective, kimeandikwa na Ha-Joon Chang. Hawa wawili wana-share a leftist leaning hasa kuhusu role ya mifumo na taasisi za kimataifa kwenye kuleta au kukandamiza maendeleo. Lakini kikubwa najifunza kwa sasa ni a remarkable history of economics itself.

Kuhusu vitabu gani na-recommend vijana wasome au mambo gani ya kutafakari na kujifunza. Hili ni gumu kidogo manake viko vitabu vingi sana ambavyo ni muhimu na mambo vilevile ni mengi kwa vijana kuzingatia.

Cha msingi ni kwamba, kwanza, kijana ni lazima awe na consciousness kama mtu, kama mwanadamu. Hapa napendekeza vitabu vya falsafa, hasa Martin Heidegger’s Being and Time (mwalimu wangu wa philosophy St. John’s, Father Rene McGraw, alikuwa mwanafunzi wa Heidegger) na philosophers wengine ambao wanakusukuma saa zote kuwa self-aware na utu wako na matendo yako. 

Pili, kijana wa Kibongo ni muhimu awe conscious kwamba yeye ni Mtanzania na azingatie the idea kwamba citizenship maana yake ni community, kwamba matendo yako yote, hata kutupa barabarani chupa tupu ya maji ya Kilimanjaro, lazima yazingatie kwamba tunaishi kwenye community, hata unapopokea simu ukiwa kwenye daladala, namna na ukubwa wa sauti unayoitumia kuongea ni suala la citizenship. Kujenga a sense of responsibility to the community ni muhimu sana kwa vijana. La sivyo tutakuwa tunaishi kama wanyama tu, kila mtu akitaka yeye ndio awahi foleni, a-divert bomba la maji mtaani liende kwake peke yake, n.k. Kitabu cha Robert Putnam, kinachoitwa Bowling Alone, kilinifungua macho kwenye masuala haya (ingawa context yake ni Marekani). 

Tatu, kijana ni muhimu ajue historia ya nchi yake na sacrifices walizochukua wazee wetu huko nyuma hadi kufikia nchi yetu ikawa huru na kuwa kama ilivyo leo. Vitabu kwa ajili ya elimu hii viko vingi sina haja ya kuviorodhesha. Nne, kijana ni lazima awe na basic idea kuhusu challenges za mahali anapoishi na angalau ajisumbue kutafakari kuhusu majawabu yake – kwa mfano, kwa sisi wa Dar es Salaam, kwa miaka kumi ijayo changamoto kubwa tatu: upatikanaji wa maji pamoja na handling ya majitaka, energy kwa kupikia na city transport. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, bei ya mkaa (cooking energy ya majority) imeongezeka kutoka shilingi 7,000 hadi shilingi 40,000 kwa gunia, radius ya eneo mkaa unakopatikana imeongezeka beyond Bagamoyo, kuelekea mapori beyond Mikumi na sasa watu wanaikwangua Selous. Mto Ruvu, source kubwa ya maji jijini Dar, inapungua volume by 6 percent every year. Kijana lazima asumbuke kutafakari haya mambo. Sio jukumu la Serikali au viongozi pekee. Tano, kijana ni lazima ajue mambo yanayoendelea duniani na kujaribu kutafuta rationale na implications za kila tukio.

Kwa ujumla, katika mambo yote haya, suala kubwa ni kuwa kuwa curious. Kijana akiwa curious atatafuta habari au atajisumbua kwa tafakuri. Mfano, ukisoma The Economist kila wiki kwa mwaka mzima ni elimu kubwa sana.

In the end, vitabu ambavyo kwa kufikiria haraka haraka huwa na-recommend kwa watu: Guns, Germs and Steel: The Fates of Human Societies by Jared Diamond; na Tuesdays with Morrie cha Mitch Albom.

Sahamani nikurudishe nyuma kidogo, wewe umesoma university Marekani na kule tunasikia college maisha ya kule ni furaha wakati wote na ni experience kubwa ambayo watu huwa hawasahau. Unaweza kutuambia mambo ambayo huwezi kusahau ulipokuwa college?

Ni kweli uliyosema, lakini yote yanategemea ni college gani mtu alienda. Kwanza, mimi nilienda college nikiwa tayari nimekwishafanya kazi kwenye kambi za wakimbizi huku Tanzania, kwahiyo ingawa nilikuwa sio mtu mzima sana, lakini nilikuwa kidogo na heshima yangu kwahiyo sikufanya sana fujo campus. Pili, college niliyoenda haikutoa sana fursa hivyo. Kilikuwa ni Chuo cha Wakatoliki in a real sense (ingawa dini nyingine walikuwa wanasoma na mtu hukulazimishwa kusoma theology na kwenda kanisani), kwa maana ya kwamba kulikuwa na Seminary pale pale lakini kubwa zaidi kulikuwa na Monastery pamoja na monks wa Benedictine na majoho yao meusi. Zaidi ya nusu ya wahadhiri wangu walikuwa monks. Kwahiyo haya mazingira yalikuwa kidogo na “utakatifu”.

Jambo ambalo siwezi kusahau college labda ni moja. Kwanza, pale College nilipata nafasi ya kufanya kazi kwenye nursing home ya monks – yaani kituo ambacho wale watawa (monks) wameshakuwa wazee sana au wagonjwa kwahiyo wamepelekwa kusubiri kufariki. Sasa, imagine saa zote umekaa na hawa watu ambao maisha yao yote wamejitolea kuwa watawa, kuwa watumishi wa mungu, halafu wewe unakuwa rafiki yao wakati wana-contemplate death na wana-reflect maisha yao yote. Mazungumzo yangu na wao, in fact mazungumzo yao ya mwisho mwisho, kuhusu faith, immortality na ethics siwezi kuyasahau.

Sina maana ya kusema maisha yangu yamekuwa ya kitakatifu milele. Nimefanya fujo za ujana huko Sekondari na High School pia. Na still I am not a perfect person, na kila siku ni siku ya jitihada ya kuwa a better person, a better father, a better husband, a better citizen, a better public servant.

Asante kwa mahojiano hayo, je ungependa kuwapa ujumbe gani vijana wenzako wa Tanzania?

70 percent of Tanzanians are under the age of 30. Umri wa wastani wa Watanzania ni miaka 18. Taifa letu ni taifa la vijana – ndio tuliojaa. Kwahiyo, kwanza, ni muhimu kwa vijana kujitokeza ku-shape the future ambayo tunaitaka - sio kwa maneno tu au kwa mijadala pekee, bali kwa vitendo. Pili, kama tunataka kujenga jamii inayo-focus kwenye mambo ya msingi ya maendeleo, pa kuanzia ni kwenye mahusiano baina yetu: tupendane, tusaidiane, tusichukiane, tusikandiane.

 

Skin 1